Zaburi 74:9
Psalms 74:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hatukupewa ishara za miujiza; hakuna manabii waliobaki, hakuna yeyote kati yetu ajuaye hali hii itachukua muda gani.
Psalms 74:9 in English
Psalms 74:9 · Berean Standard Bible
There are no signs for us to see. There is no longer any prophet. And none of us knows how long this will last.
Context
7Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako. 8Walisema mioyoni mwao,
“Tutawaponda kabisa!”
Walichoma kila mahali ambapo Mungu
aliabudiwa katika nchi. 9Hatukupewa ishara za miujiza;
hakuna manabii waliobaki,
hakuna yeyote kati yetu ajuaye
hali hii itachukua muda gani. 10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?
Je, adui watalitukana jina lako milele? 11Kwa nini unazuia mkono wako,
mkono wako wa kuume?
Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako
na uwaangamize!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.