Zaburi 72:15
Psalms 72:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa.
Psalms 72:15 in English
Psalms 72:15 · Berean Standard Bible
Long may he live! May gold from Sheba be given him. May people ever pray for him; may they bless him all day long.
Context
13Atawahurumia wanyonge na wahitaji
na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. 14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,
kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. 15Aishi maisha marefu!
Na apewe dhahabu ya Sheba.
Watu wamwombee daima
na kumbariki mchana kutwa. 16Nafaka ijae tele katika nchi yote,
juu ya vilele vya vilima na istawi.
Tunda lake na listawi kama Lebanoni,
listawi kama majani ya kondeni. 17Jina lake na lidumu milele,
na lidumu kama jua.
Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,
nao watamwita aliyebarikiwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.