Zaburi 69:5
Psalms 69:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.
Psalms 69:5 in English
Psalms 69:5 · Berean Standard Bible
You know my folly, O God, and my guilt is not hidden from You.
Context
3Nimechoka kwa kuomba msaada,
koo langu limekauka.
Macho yangu yanafifia,
nikimtafuta Mungu wangu. 4Wale wanaonichukia bila sababu
ni wengi kuliko nywele za kichwa changu;
wengi ni adui kwangu bila sababu,
wale wanaotafuta kuniangamiza.
Ninalazimishwa kurudisha
kitu ambacho sikuiba. 5Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu,
wala hatia yangu haikufichika kwako. 6Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
wakutumainio wasiaibishwe
kwa ajili yangu;
wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu,
Ee Mungu wa Israeli. 7Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako,
aibu imefunika uso wangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.