Native Bible

Psalms 69:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.

Psalms 69:3 in English

Psalms 69:3 · Berean Standard Bible

I am weary from my crying; my throat is parched. My eyes fail, looking for my God.

Context

1Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. 2Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha. 3Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. 4Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba. 5Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.