Native Bible

Psalms 68:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi.

Psalms 68:21 in English

Psalms 68:21 · Berean Standard Bible

Surely God will crush the heads of His enemies, the hairy crowns of those who persist in guilty ways.

Context

19Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. 20Mungu wetu ni Mungu aokoaye, Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo. 21Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi. 22Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, 23ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.