Native Bible

Psalms 65:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ewe usikiaye maombi, kwako wewe watu wote watakuja.

Psalms 65:2 in English

Psalms 65:2 · Berean Standard Bible

O You who listen to prayer, all people will come to You.

Context

1Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. 2Ewe usikiaye maombi, kwako wewe watu wote watakuja. 3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu. 4Heri wale uliowachagua na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, mema ya Hekalu lako takatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.