Zaburi 65:3
Psalms 65:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu.
Psalms 65:3 in English
Psalms 65:3 · Berean Standard Bible
When iniquities prevail against me, You atone for our transgressions.
Context
1Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni;
kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. 2Ewe usikiaye maombi,
kwako wewe watu wote watakuja. 3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi,
wewe ulisamehe makosa yetu. 4Heri wale uliowachagua
na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako!
Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako,
mema ya Hekalu lako takatifu. 5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki,
Ee Mungu Mwokozi wetu,
tumaini la miisho yote ya duniani
na la bahari zilizo mbali sana,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.