Native Bible

Psalms 57:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.

Psalms 57:3 in English

Psalms 57:3 · Berean Standard Bible

He reaches down from heaven and saves me; He rebukes those who trample me. Selah God sends forth His loving devotion and His truth.

Context

1Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. 2Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 4Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali. 5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.