Zaburi 57:2
Psalms 57:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.
Psalms 57:2 in English
Psalms 57:2 · Berean Standard Bible
I cry out to God Most High,* to God who fulfills His purpose for me.
Context
1Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie,
kwa maana nafsi yangu inakukimbilia.
Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia
mpaka maafa yapite. 2Namlilia Mungu Aliye Juu Sana,
Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa,
akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali;
Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 4Niko katikati ya simba,
nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu:
watu ambao meno yao ni mikuki na mishale,
ambao ndimi zao ni panga kali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.