Zaburi 49:13
Psalms 49:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
Psalms 49:13 in English
Psalms 49:13 · Berean Standard Bible
This is the fate of the self-confident * and their followers who endorse their sayings. Selah
Context
11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele,
makao yao vizazi vyote;
ingawa walikuwa na mashamba
na kuyaita kwa majina yao. 12Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu;
anafanana na mnyama aangamiaye. 13Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe,
pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. 14Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini,*
nacho kifo kitawala.
Wanyofu watawatawala asubuhi,
maumbile yao yataozea kaburini,
mbali na majumba yao makubwa ya fahari. 15Lakini Mungu atakomboa uhai* wangu na kaburi,
hakika atanichukua kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.