Zaburi 40:13
Psalms 40:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
Psalms 40:13 in English
Psalms 40:13 · Berean Standard Bible
Be pleased, O LORD, to deliver me; hurry, O LORD, to help me.
Context
11Ee Bwana, usizuilie huruma zako,
upendo wako na kweli yako daima vinilinde. 12Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,
dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.
Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,
nao moyo unazimia ndani yangu. 13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie. 14Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu. 15Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
wafadhaishwe na iwe aibu yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.