Native Bible

Psalms 40:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

Psalms 40:11 in English

Psalms 40:11 · Berean Standard Bible

O LORD, do not withhold Your mercy from me; Your loving devotion and faithfulness will always guard me.

Context

9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo. 10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa. 11Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde. 12Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu. 13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.