Zaburi 37:18
Psalms 37:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.
Psalms 37:18 in English
Psalms 37:18 · Berean Standard Bible
The LORD knows the days of the blameless, and their inheritance will last forever.
Context
16Bora kidogo walicho nacho wenye haki
kuliko wingi wa mali wa waovu wengi; 17kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa,
lakini Bwana humtegemeza mwenye haki. 18Bwana anazifahamu siku za wanyofu,
na urithi wao utadumu milele. 19Siku za maafa hawatanyauka,
siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. 20Lakini waovu wataangamia:
Adui za Bwana watakuwa
kama uzuri wa mashamba,
watatoweka,
watatoweka kama moshi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.