Zaburi 35:20
Psalms 35:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi.
Psalms 35:20 in English
Psalms 35:20 · Berean Standard Bible
For they do not speak peace, but they devise deceitful schemes against those who live quietly in the land.
Context
18Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
nitakusifu katikati ya watu wengi. 19Usiwaache wale wanaonisimanga,
wale ambao ni adui zangu bila sababu;
usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu
wakonyeze jicho kwa hila. 20Hawazungumzi kwa amani,
bali wanatunga mashtaka ya uongo
dhidi ya wale wanaoishi
kwa utulivu katika nchi. 21Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha!
Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” 22Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya.
Usiwe mbali nami, Ee Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.