Native Bible

Psalms 35:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Bwana, utatazama mpaka lini? Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, uhai wangu wa thamani kutokana na simba hawa.

Psalms 35:17 in English

Psalms 35:17 · Berean Standard Bible

How long, O Lord, will You look on? Rescue my soul from their ravages, my precious life from these lions.

Context

15Lakini nilipojikwaa, walikusanyika kwa shangwe; washambuliaji walijikusanya dhidi yangu bila mimi kujua. Walinisingizia pasipo kukoma. 16Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, wamenisagia meno. 17Ee Bwana, utatazama mpaka lini? Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, uhai wangu wa thamani kutokana na simba hawa. 18Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi. 19Usiwaache wale wanaonisimanga, wale ambao ni adui zangu bila sababu; usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu wakonyeze jicho kwa hila.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.