Zaburi 18:7
Psalms 18:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
Psalms 18:7 in English
Psalms 18:7 · Berean Standard Bible
Then the earth shook and quaked, and the foundations of the mountains trembled; they were shaken because He burned with anger.
Context
5Kamba za kuzimu zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili. 6Katika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu anisaidie.
Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika mbele zake,
masikioni mwake. 7Dunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya milima ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 8Moshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake. 9Akazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.