Native Bible

Psalms 18:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili.

Psalms 18:5 in English

Psalms 18:5 · Berean Standard Bible

The cords of Sheol entangled me; the snares of death confronted me.

Context

3Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 4Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 5Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. 6Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake. 7Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.