Native Bible

Psalms 18:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.

Psalms 18:8 in English

Psalms 18:8 · Berean Standard Bible

Smoke rose from His nostrils, and consuming fire came from His mouth; glowing coals blazed forth.

Context

6Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake. 7Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 8Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. 9Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 10Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.