Native Bible

Psalms 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?”

Psalms 11:3 in English

Psalms 11:3 · Berean Standard Bible

If the foundations are destroyed, what can the righteous do?”

Context

1Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako. 2Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo. 3Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?” 4Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. 5Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.