Native Bible

Psalms 109:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya.

Psalms 109:20 in English

Psalms 109:20 · Berean Standard Bible

May this be the LORD’s reward to my accusers, to those who speak evil against me.

Context

18Alivaa kulaani kama vazi lake, nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, kwenye mifupa yake kama mafuta. 19Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima. 20Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya. 21Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako. 22Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.