Zaburi 104:27
Psalms 104:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake.
Psalms 104:27 in English
Psalms 104:27 · Berean Standard Bible
All creatures look to You to give them their food in due season.
Context
25Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele,
imejaa viumbe visivyo na idadi,
vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. 26Huko meli huenda na kurudi,
pia Lewiathani,* uliyemuumba acheze ndani yake. 27Hawa wote wanakutazamia wewe,
uwape chakula chao kwa wakati wake. 28Wakati unapowapa,
wanakikusanya,
unapofumbua mkono wako,
wao wanashibishwa mema. 29Unapoficha uso wako,
wanapata hofu,
unapoondoa pumzi yao,
wanakufa na kurudi mavumbini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.