Native Bible

Psalms 104:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani,* uliyemuumba acheze ndani yake.

Psalms 104:26 in English

Psalms 104:26 · Berean Standard Bible

There the ships pass, and Leviathan, which You formed to frolic there.

Context

24Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. 25Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. 26Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani,* uliyemuumba acheze ndani yake. 27Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. 28Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.