Mithali 4:13
Proverbs 4:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima wako.
Proverbs 4:13 in English
Proverbs 4:13 · Berean Standard Bible
Hold on to instruction; do not let go. Guard it, for it is your life.
Context
11Ninakuongoza katika njia ya hekima
na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka. 12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa;
ukimbiapo, hutajikwaa. 13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
mshike, maana yeye ni uzima wako. 14Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu
wala usitembee katika njia ya watu wabaya. 15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo;
achana nayo, na uelekee njia yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.