Native Bible

Proverbs 28:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini.

Proverbs 28:8 in English

Proverbs 28:8 · Berean Standard Bible

He who increases his wealth by interest and usury lays it up for one who is kind to the poor.

Context

6Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu. 7Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. 8Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. 9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo. 10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.