Mithali 28:11
Proverbs 28:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.
Proverbs 28:11 in English
Proverbs 28:11 · Berean Standard Bible
A rich man is wise in his own eyes, but a poor man with discernment sees through him.
Context
9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria,
hata maombi yake ni chukizo. 10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya,
ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe,
bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. 11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe,
bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa,
bali waovu watawalapo, watu hujificha. 13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,
bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.