Mithali 28:13
Proverbs 28:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.
Proverbs 28:13 in English
Proverbs 28:13 · Berean Standard Bible
He who conceals his sins will not prosper, but whoever confesses and renounces them will find mercy.
Context
11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe,
bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa,
bali waovu watawalapo, watu hujificha. 13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,
bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 14Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,
bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu
huangukia kwenye taabu. 15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye,
ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.