Native Bible

Proverbs 28:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha.

Proverbs 28:12 in English

Proverbs 28:12 · Berean Standard Bible

When the righteous triumph, there is great glory, but when the wicked rise, men hide themselves.

Context

10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. 11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. 13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 14Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.