Native Bible

Proverbs 25:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa.

Proverbs 25:15 in English

Proverbs 25:15 · Berean Standard Bible

Through patience a ruler can be persuaded, and a gentle tongue can break a bone.

Context

13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake. 14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. 15Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa. 16Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, ukila zaidi, utatapika. 17Ingiza mguu wako nyumbani kwa jirani yako mara chache, ukizidisha, atakukinai na atakuchukia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.