Native Bible

Proverbs 25:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi.

Proverbs 25:14 in English

Proverbs 25:14 · Berean Standard Bible

Like clouds and wind without rain is the man who boasts of gifts never given.

Context

12Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. 13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake. 14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. 15Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa. 16Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, ukila zaidi, utatapika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.