Mithali 25:13
Proverbs 25:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake.
Proverbs 25:13 in English
Proverbs 25:13 · Berean Standard Bible
Like the cold of snow in the time of harvest is a trustworthy messenger to those who send him; he refreshes the soul of his masters.
Context
11Neno lisemwalo kwa wakati ufaao
ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu
yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. 12Kama vile kipuli cha dhahabu
au pambo la dhahabu safi,
ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima
kwa sikio lisikilizalo. 13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno
ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao,
huburudisha roho za bwana zake. 14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua
ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. 15Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa,
nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.