Native Bible

Proverbs 25:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha.

Proverbs 25:11 in English

Proverbs 25:11 · Berean Standard Bible

A word fitly spoken is like apples of gold in settings of silver.

Context

9Kama ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine, 10ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. 11Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. 12Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. 13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.