Mithali 16:23
Proverbs 16:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.
Proverbs 16:23 in English
Proverbs 16:23 · Berean Standard Bible
The heart of the wise man instructs his mouth and adds persuasiveness to his lips.
Context
21Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu,
na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho. 22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao,
bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu. 23Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake,
na midomo yake huchochea mafundisho. 24Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali,
ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. 25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
bali mwisho wake huelekeza mautini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.