Hesabu 7:13
Numbers 7:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,* na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,* vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
Numbers 7:13 in English
Numbers 7:13 · Berean Standard Bible
His offering was one silver platter weighing a hundred and thirty shekels,* and one silver bowl weighing seventy shekels,* both according to the sanctuary shekel and filled with fine flour mixed with oil for a grain offering;
Context
11Kwa maana Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.” 12Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda. 13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,* na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,* vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 14sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi,* likiwa limejazwa uvumba; 15fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.