Native Bible

Numbers 7:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

Numbers 7:12 in English

Numbers 7:12 · Berean Standard Bible

On the first day Nahshon son of Amminadab from the tribe of Judah drew near with his offering.

Context

10Wakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. 11Kwa maana Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.” 12Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda. 13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,* na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,* vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 14sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi,* likiwa limejazwa uvumba;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.