Hesabu 7:15
Numbers 7:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
Numbers 7:15 in English
Numbers 7:15 · Berean Standard Bible
one young bull, one ram, and one male lamb a year old for a burnt offering;
Context
13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,* na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,* vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 14sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi,* likiwa limejazwa uvumba; 15fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 16mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 17maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.