Hesabu 11:32
Numbers 11:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.* Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote.
Numbers 11:32 in English
Numbers 11:32 · Berean Standard Bible
All that day and night, and all the next day, the people stayed up gathering the quail. No one gathered less than ten homers,* and they spread them out all around the camp.
Context
30Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini. 31Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande. 32Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.* Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote. 33Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni. 34Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava,* kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.