Native Bible

Numbers 11:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni.

Numbers 11:33 in English

Numbers 11:33 · Berean Standard Bible

But while the meat was still between their teeth, before it was chewed, the anger of the LORD burned against the people, and the LORD struck them with a severe plague.

Context

31Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande. 32Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.* Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote. 33Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni. 34Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava,* kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine. 35Kutoka Kibroth-Hataava watu wakasafiri mpaka Haserothi na kukaa huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.