Hesabu 11:30
Numbers 11:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini.
Numbers 11:30 in English
Numbers 11:30 · Berean Standard Bible
Then Moses returned to the camp, along with the elders of Israel.
Context
28Yoshua mwana wa Nuni, ambaye alikuwa msaidizi wa Mose tangu ujana wake, akajibu akasema, “Mose bwana wangu, wanyamazishe!” 29Lakini Mose akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote wa Bwana wangekuwa manabii na kwamba Bwana angeweka Roho yake juu yao!” 30Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini. 31Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande. 32Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.* Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.