Native Bible

Numbers 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,* kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao.

Numbers 11:3 in English

Numbers 11:3 · Berean Standard Bible

So that place was called Taberah,* because the fire of the LORD had burned among them.

Context

1Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 2Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika. 3Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,* kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao. 4Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! 5Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.