Hesabu 11:4
Numbers 11:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule!
Numbers 11:4 in English
Numbers 11:4 · Berean Standard Bible
Meanwhile, the rabble among them had a strong craving for other food, and again the Israelites wept and said, “Who will feed us meat?
Context
2Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika. 3Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,* kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao. 4Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! 5Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu. 6Lakini sasa tumepoteza hamu ya chakula; hatuoni kitu kingine chochote isipokuwa hii mana!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.