Native Bible

Numbers 11:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.

Numbers 11:1 in English

Numbers 11:1 · Berean Standard Bible

Soon the people began to complain about their hardship in the hearing of the LORD, and when He heard them, His anger was kindled, and fire from the LORD blazed among them and consumed the outskirts of the camp.

Context

1Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 2Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika. 3Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,* kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.