Native Bible

Numbers 10:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

Numbers 10:27 in English

Numbers 10:27 · Berean Standard Bible

and Ahira son of Enan was over the division of the tribe of Naphtali.

Context

25Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao. 26Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri, 27naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali. 28Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka. 29Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo Bwana amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana Bwana ameahidi mambo mema kwa Israeli.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.