Hesabu 10:25
Numbers 10:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.
Numbers 10:25 in English
Numbers 10:25 · Berean Standard Bible
Finally, the divisions of the camp of Dan set out under their standard, serving as the rear guard for all units, with Ahiezer son of Ammishaddai in command.
Context
23Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase, 24naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini. 25Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao. 26Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri, 27naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.