Hesabu 1:17
Numbers 1:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,
Numbers 1:17 in English
Numbers 1:17 · Berean Standard Bible
So Moses and Aaron took these men who had been designated by name,
Context
15kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.” 16Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli. 17Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao, 18wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, 19kama Bwana alivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.