Native Bible

Nahum 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Chukueni nyara za fedha! Chukueni nyara za dhahabu! Wingi wake hauna mwisho, utajiri kutoka hazina zake zote!

Nahum 2:9 in English

Nahum 2:9 · Berean Standard Bible

“Plunder the silver! Plunder the gold!” There is no end to the treasure, an abundance of every precious thing.

Context

7Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe na upelekwe uhamishoni. Vijakazi wake wanaomboleza kama hua na kupigapiga vifua vyao. 8Ninawi ni kama dimbwi, nayo maji yake yanakauka. Wanalia, “Simama! Simama!” Lakini hakuna anayegeuka nyuma. 9Chukueni nyara za fedha! Chukueni nyara za dhahabu! Wingi wake hauna mwisho, utajiri kutoka hazina zake zote! 10Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi! Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea, miili inatetemeka, na kila uso umebadilika rangi. 11Liko wapi sasa pango la simba, mahali ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walikwenda na ambapo wana simba walikwenda bila kuogopa chochote?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.