Nahumu 2:10
Nahum 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi! Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea, miili inatetemeka, na kila uso umebadilika rangi.
Nahum 2:10 in English
Nahum 2:10 · Berean Standard Bible
She is emptied! Yes, she is desolate and laid waste! Hearts melt, knees knock, bodies tremble, and every face grows pale!
Context
8Ninawi ni kama dimbwi,
nayo maji yake yanakauka.
Wanalia, “Simama! Simama!”
Lakini hakuna anayegeuka nyuma. 9Chukueni nyara za fedha!
Chukueni nyara za dhahabu!
Wingi wake hauna mwisho,
utajiri kutoka hazina zake zote! 10Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi!
Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea,
miili inatetemeka,
na kila uso umebadilika rangi. 11Liko wapi sasa pango la simba,
mahali ambapo waliwalisha watoto wao,
ambapo simba dume na simba jike walikwenda
na ambapo wana simba walikwenda
bila kuogopa chochote? 12Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake,
alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake,
akijaza makao yake kwa alivyoua
na mapango yake kwa mawindo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.