Nahumu 2:8
Nahum 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninawi ni kama dimbwi, nayo maji yake yanakauka. Wanalia, “Simama! Simama!” Lakini hakuna anayegeuka nyuma.
Nahum 2:8 in English
Nahum 2:8 · Berean Standard Bible
Nineveh has been like a pool of water throughout her days, but now it is draining away. “Stop! Stop!” they cry, but no one turns back.
Context
6Malango ya mto yamefunguliwa wazi,
na jumba la kifalme limeanguka. 7Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe
na upelekwe uhamishoni.
Vijakazi wake wanaomboleza kama hua
na kupigapiga vifua vyao. 8Ninawi ni kama dimbwi,
nayo maji yake yanakauka.
Wanalia, “Simama! Simama!”
Lakini hakuna anayegeuka nyuma. 9Chukueni nyara za fedha!
Chukueni nyara za dhahabu!
Wingi wake hauna mwisho,
utajiri kutoka hazina zake zote! 10Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi!
Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea,
miili inatetemeka,
na kila uso umebadilika rangi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.