Nahumu 2:6
Nahum 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Malango ya mto yamefunguliwa wazi, na jumba la kifalme limeanguka.
Nahum 2:6 in English
Nahum 2:6 · Berean Standard Bible
The river gates are thrown open and the palace collapses.
Context
4Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani,
yakikimbia nyuma na mbele uwanjani.
Yanaonekana kama mienge ya moto;
yanakwenda kasi kama umeme. 5Anaita vikosi vilivyochaguliwa,
lakini bado wanajikwaa njiani.
Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji,
ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. 6Malango ya mto yamefunguliwa wazi,
na jumba la kifalme limeanguka. 7Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe
na upelekwe uhamishoni.
Vijakazi wake wanaomboleza kama hua
na kupigapiga vifua vyao. 8Ninawi ni kama dimbwi,
nayo maji yake yanakauka.
Wanalia, “Simama! Simama!”
Lakini hakuna anayegeuka nyuma.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.