Native Bible

Nahum 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani, yakikimbia nyuma na mbele uwanjani. Yanaonekana kama mienge ya moto; yanakwenda kasi kama umeme.

Nahum 2:4 in English

Nahum 2:4 · Berean Standard Bible

The chariots dash through the streets; they rush around the plazas, appearing like torches, darting about like lightning.

Context

2Bwana atarudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa na wameharibu mizabibu yao. 3Ngao za askari wake ni nyekundu, mashujaa wamevaa nguo nyekundu. Chuma kwenye magari ya vita chametameta, katika siku aliyoyaweka tayari, mikuki ya mierezi inametameta. 4Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani, yakikimbia nyuma na mbele uwanjani. Yanaonekana kama mienge ya moto; yanakwenda kasi kama umeme. 5Anaita vikosi vilivyochaguliwa, lakini bado wanajikwaa njiani. Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. 6Malango ya mto yamefunguliwa wazi, na jumba la kifalme limeanguka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.