Native Bible

Nahum 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ngao za askari wake ni nyekundu, mashujaa wamevaa nguo nyekundu. Chuma kwenye magari ya vita chametameta, katika siku aliyoyaweka tayari, mikuki ya mierezi inametameta.

Nahum 2:3 in English

Nahum 2:3 · Berean Standard Bible

The shields of his mighty men are red; the valiant warriors are dressed in scarlet. The fittings of the chariots flash like fire on the day they are prepared, and the spears of cypress have been brandished.*

Context

1Mshambuliaji anasogea dhidi yako, Ninawi. Linda ngome, chunga barabara, jitieni nguvu wenyewe, kusanya nguvu zako zote! 2Bwana atarudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa na wameharibu mizabibu yao. 3Ngao za askari wake ni nyekundu, mashujaa wamevaa nguo nyekundu. Chuma kwenye magari ya vita chametameta, katika siku aliyoyaweka tayari, mikuki ya mierezi inametameta. 4Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani, yakikimbia nyuma na mbele uwanjani. Yanaonekana kama mienge ya moto; yanakwenda kasi kama umeme. 5Anaita vikosi vilivyochaguliwa, lakini bado wanajikwaa njiani. Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.